social facebook box instragram-icon you-tube-logo social-google-plus social twitter slideshare-icon

Maelezo Mafupi Kuhusu Nyoka

By Sanda Ashe.

KUMBUKA!
Usichelewe kuona daktari!
Usijaribu kutumia dawa usiyoijua matumizi yake!
Usifunge kamba ama nyuzi kwa mguu ama mkono ulioumwa na nyoka!
Usiruhusu kyumia stima ama dawa mahali palipoumwa na nyoka!

Ukiwa Shambani au Njiani
Unaweza kuuliza maswali kama vile
Jinsi ya Kutibu Aliyetemewa Sumu kwa Macho na Nyoka
Hatua Rahisi za Kuishi kwa Usalama Katika Maeneo ya Nyoka Wengi

Ukiwa Shambani au Njiani:
- Ikiwa yule nyoka aliyekuuma utamuua, basi ni vyema pia umuweke mahali pazuri hadi kwa daktari. Lakini kama nyoka hukumuona wakati wa ajali, wewe usipoteze wakati ukimtafuta. Ni bizuru utafute njia ya kumsaidia yule aliye pata ajali kwa njia ya harak iwezekanavyo.
- Wakati wa ajali yoyote kama hasara ya kuumwa na nyoka ni vizuri yule msadizi au muhuduma yeyote awe mtulivu na mwenye kutia moyo kwa aliyepata ajali hiyo. Si vizuri kuruhusu wapita njia au watu wenine wa jamii wenye kubabaika wanapona ajali kama hii, kukaa karibu na mgonjwa. Mara nyingi wata huzidiwa na hali mbaya na mara nyengine hufa kwa sababu ya kutiwa hofu na wasiwasi. Wakati was ajali kama hii, yakupasa uwe mtu wa kujipa moyo. Usiruhusu watu wakutie hofu hata nyoka awe mkubwa kiasi gani.
- Mtu aliye pata hasara kama hii anapaswa kusaidiwa kwa kuondo vitu vyovyote kama sa ya mkono, bangili, ama hata nguo ambayo inamshika sana. Wakati ukifanya harakati za kumpeleka aliyeumwa na nyoka kwa daktari, hakikisha ule mguu au mkono ule ulio umwa umezuiliwa na kama vile kipande cha nguo. Kinyume na desturi, usimfunge kitu chochote iwe ni mkono au mguu ulioumwa. Unapofunga mahali palipo umwa unazuia damu kuzunguku mwilini. Hivyo basi athari za ile sumu husababisha uharibifu mkubwa katika mguu au mkono ule. Mara nyingi damu inapokosa kuzunguka vizuri, mguu hufura zaidi.
- Hakikisha kwamba wakati munapoenda kwa daktari, unajaribu kujua habari muhimu kuhusu aina ya yule nyoke. Hivyo utasadia kutoa habari muhimu kwa haraka ikiwa yule mgonjwa atakuwa hali mbaya ya kushindwa kupeana maelezo mwenyewe.
- Ni vizuri kuhakikisha ya kwamba unafahamu ni wapi unaweza kupata dawa ya kipekee ya aina ya 'Antivenom'. Jua ya kwamba dawa hii ya nyoka iliyo ya kipekee, ni bei ghali na kwa hivyo si rahisi kupatikana katika hospitali ndogo ama maduka yote ya dawa, Ushauri wangu ni kwamba watu wa kijiji waweza kujiunga na kununua dawa hizi na kuweka mahali palipo na 'refrigerator' kwa manufaa ya watuwa kijiji chote.
- Kuwa makini wakati unasafiri hospitali. Ikiwa uchunu unazidi unaweza kutumia dawa aina ya Panadol. Kumbuka ya kwamba damu inapokuwa haizunguki kwa mwendo wa sawa mwilini yawezakuwa sababu ya kumfanya mgonjwa azirai. Wakati amezirai, wewe unaweza kusaidia kwa kuinua miguu yake hadi hali ya usalama imurudie huyo mgonjwa.
- Mara nyingine nyoka anaweza hata kusababisha kidondo kikubwa. Uispokuwa na tahadhari basi mahali plae paweza kusabbabisha mguu ukatwe au hata kifo. Vidonda vya aina hii visipochunguzwa na daktari na kutunzwa vizuri, mwishowe huwa donda ndugu na vyaweza kupozesha mguu.

Unaweza kuuliza maswali kama vile:
- Uliona nyoka aliyekuuma. Alikuwa yuko namna gani.
- Alitoa sauti gani? Alitupa mate au alitoa ulimi wa panda?
- Ulikuwa kwa manyasi au juu ya mti wakati uliumwa au kwa nyumba?
- Uliumwa saa ngapi?
- Jee, umekunywa pombe ama dawa yoyote kabia ya kuumwa na nyoka?

Jinsi ya Kutibu Alieyetemewa Sumu kwa Macho na Nyoka
- Ikiwa yule nyoka mate kwa macho, basi osha macho yako kwa maji mengi. Lakini, mahali hakuna hata maji, unaweza kutumia mkojo safi kuosha macho pekee. Kila sehemu ya mwili iliyomwagikiwa na sumu lazima ioshwe vizuri.
- Lile jicho liloathiriwa huenda likawasha kwa muda na hata pia kutokwa na machozi huku pia mate yakijaa mdomoni.
- Pangusa kutumia kitambaa safi kuelekea nje ya kicho, ili usiruhusu sumu kurudi ndani ya jicho.
- Kumbuka ya kwamba sio nyoka wote wana sumu.
- Hakikisha ya kwamba mgonjwa anapata chakula kilicho na maji mengi.
- Ikiwa mgonjwa anashida ya kupata mkojo, tafadhali umpeleke kwa daktari.
Wakati huu anopoendelea kupata nafuu mgonjwa anaweza kuhisi uchovu ama hata pia kuzirai. Ni vizuri awe na mahali pazuri pa kujituliza.
- Kama mahali palipoumwa panatoka damu, kidonda hicho lazima kiaguliwe kwa hali ya usafi, kulingana na maagizo ya daktari hadi mgonwa apone. Vidonda kama hivyo vyaweza kuleta madhara makubwa kiasi cha kumfanya mtu kuwa kiwete au kukatwa mkono. Kwa hivyo nivizuri kujifunza kujua jinsi ya kuepuka janga kama hili.

Kumbuka kwamba sumu ya nyoka huwasha sana kwa macho, kwa hivyo kuwa na huruma lakini usiogope kuendelea kotoa usaidizi kwa mgonjwa huyo. Baada ya kutoa huduma ya kwanza ni sharti mgonjwa kuona daktari kukagua jicho hilo kwa undani zaidi.

Hatua Rahisi za Kuishi kwa Usalam Katika Maeneo ya Nyoka Wengi:
Kumbuka kwamba nyoka wote ni hatari. Hata hivyo, mara nyingi huishi kwa kuua wanyama wadogo, kama vile panya, hivyo basi kuzuia kuenezwa kwa magonjwa mengineyo. Wao pia hula aina ya denge ambao poa wakiwa wengi mno huleta uharibifu kwa memea shambani. Ninakushauri kwamba, ujaribu uwezavyo kuona ya kwamba, ujaribu uwezavyo kuona ya kwamba si kila nyoka unayemuona njiani astahili kuuliwa. Ni vizuri kuwatunza kiasi kama raslimali asili ya dunia hii. Lakini tujihadhari sana kwani aina chache za nyoka wanayo sumu kali inayoweza kuhatarisha maish yako, kwa hivyo ni vizuri tuzingatiye maelezo machache yafuatayo.
- Ukiwa kwa boma lako, jaribu sana kujenga kibanda cha migugo, sana kibanda cha kuku na bata au hata sungura.
- Jaribu iwezekanavyo kuweka chakula mahali ambapo panya hawawezi kufanya makao kwa sababu nyoka ataingia ndani kwa kutaka kuwala.
- Jaribu kuhakikisha mahali pa kulala kumeinuliwa juu, huku ikiwezekana, pia utumie 'neti wa umbu'.
- Safisha manyasi marefu kando ya nyuma yako. Pia si vizuri kuweka mrundo mkubwa kwa kuni karibu na nyumba ya kulala, wkani hivyo ni kuwajengea mahali pa kulala wale nyoka.
- Pia si vyema kuwa na miti ya kivuli ikillalia nyumba kwani nyoka pia hupenda sehemu za utulivu kama hizo.
- Kuku na wanyama wengine wa nyumbani hutoa mlio fulani wa kutahadharisha kitu kisicho cha kawaida. Kwa hivyo chinguza uonapo mifugo wako wakionyesha kitendo kisicho cha kawaida.
- Usiweke mkono wako ndani ya msahimo, bila kujua ni wanyama aina gani wanaoishi hapo ndani.
- Kuwa makini wakati unaposafisha msitu shambani mwako. La muhimu ni kwamba iwapo utaumwa na nyka wakati wowote jaribu kufika kwa daktari haraka iwezehanavyo.